Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara Mambo ya Ndani yaingilia migogoro wakulima, wafugaji

Jumanne Sagini Wizara Mambo ya Ndani yaingilia migogoro wakulima wafugaji

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imelitaka jeshi la polisi mikoa ya Lindi na Mtwara kuwabaini na kuwachukulia hatua vinara wa migogoro kati ya wakulima na wafungaji katika mikoa hiyo.

Sambamba na hilo, wizara hiyo imewataka wasimamizi wa sheria kusimamia sheria na mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro kati ya wakulima na wafungaji.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ametoa maagizo hayo wakati akifungua maonesho ya Nanenane 2023 Kanda ya Kusini ambayo yanafanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

"Wasimamizi wa sheria hasa jeshi polisi kuwa imara katika kubaini na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaonekana kuwa ni vinara ya migogoro," amesema.

Sagina amewataka pia jeshi hilo, viongozi wa vijiji, kata na wilaya kuwa imara katika kusimamia sheria na mipango ya matumizi bora ya ardhi kuepusha migogoro ya wakulima na wafungaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live