Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wilaya ya Morogoro yapokea mradi kuwawezesha wanawake

Wilaya ya Morogoro yapokea mradi kuwawezesha wanawake

Thu, 14 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Tanzania imepokea mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwajengea elimu na fikra za kuwa wajasiriamali na kusimama pekee yaoili kujikomboa kiuchumi.

Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo, Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Rehema Bwasi amesema kuwa wamepokea kwa mikono miwili mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwajengea elimu na fikra za kuwa wajasiriamali.

Bwasi ametaja shirika lisilo la kiserikali la TGNP Mtandao kuwa ndio wataowezesha wanawake hao katika kata tatu za Bwakila Chini, Mngazi na Kisaki ambazo zina vituo vya kutoa taarifa na maarifa katika halmashauri hiyo.

“Lengo la hawa TGNP Mtandao ni kutoa elimu ya kuwawezesha wanawake kiuchumu na kuwajengea elimu na fikra za kuwa wajasilimali katika mradi huu na elimu ya ujasiliamali imekuwa kwa wananchi hususani wa vijijini umekuwa mgumu kupata elimu iko mbali nao.”alisema Bwasi.

Bwasi alisema kuwa elimu hiyo itawafungua ubongo juu ya elimu hiyo kutokana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika shughuli za uzalishaji mali zenye tija katika kujiletea maendeleo.

Ofisa maendeleo halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Florence Mwambene alisema kuwa mradi huo wa TGNP Mtandao ni mwendelezo wa miradi mbalimbali inayoelekezwa katika halmashauri hiyo.

“TGNP Mtandao sio shirika geni kwetu, hasa kwa kutuletea miradi mbalimbali kwa jamii yetu, halmashauri yetu imepata tuzo kwa kuwa na bajeti yenye mlengo wa kijinsia katika  mwaka wa fedha wa 2019/2020.”alisema Mwambene.

Mwambene amesema kuwa halmashauri hiyo imekuwa ikishirikiana na wafanyakazi wa kujitolea kutoka vituo vya taarifa na maarifa katika kuchambua bajeti ya mwaka 2019/2020 na mapendekezo yao waliyoibuliwa ngazi ya jamii yamepewa kipaumbele.

“Katika mchakato wa awali wa kupata wagombea katika nafasi za wajumbe na wenyeviti wa serikali za mitaa katika ngazi ya vijiji na vitongoji wanawake 60 na vijana imefanikiwa kuwashawishi makundi hayo kujitokeza kutia nia kugombea nafasi hizo katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa 2019.”alisema Mwambene.

Mshauri mwelekezi wa mradi huo kutoka TGNP Mtandao, Joseph Massimba amesema kuwa mradi huo una ajenda tatu ya kuwajengea uwezo kama walivyojengewa uwezo katika vituo vya maarifa na taari ya kupambana na ukali.

Massimba amesema kuwa katika mradi huo wanawake watajengewa uwezo wa kubuni, kufikiri, kushauri na uanzishwaji wa miradi midogomidogo ya mtu mmoja mmoja na kituo chenyewe ili kuwa na chanzo cha kupata fedha.

“Tunataka hivi vituo viwe na uwezo wa kuchangia kwa kutoa elimu na maarifa na taarifa za kijasiliamali za kibiashara kutoka mtu mmoja mmoja ili waweze kunufaika kupitia huu mradi.”alisema Massimba.

Diwani wa kata ya Mkambarani, Mohamed Mzee amesema kuwa mradi huo utasaidia kuwainua kiuchumi wanawake na vijana na kuwa chachu ya kusukuma gurudumu la maendeleo.

Mzee amesema kuwa baada ya kuanza kwa kata za awali, waratibu kutoka TGNP Mtandao watumie macho kwa kata ambazo zipo pembezoni hasa kata zilizopo milimani ambazo wananchi wake wamekuwa wakipitwa na fursa nyingi.

Chanzo: mwananchi.co.tz