Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wiki ya uhasibu Tanzania kufanyika Dar, wanawake na watoto waitwa kuhudhuriaanawake na watoto waitwa kuhudhuria

Wiki ya uhasibu Tanzania kufanyika Dar, wanawake na watoto waitwa kuhudhuria

Mon, 3 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wajasiriamali, wafanyabiashara, wafanyakazi, wafugaji, wavuvi na taasisi mbalimbali za biashara nchini Tanzania watapatiwa ushauri na elimu kuhusu uhasibu katika lengo la kukuza uchumi wa viwanda na maendeleo ya jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 3, 2020 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA), Peter Mwambuja amesema TAA kwa kushirikiana na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) na Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) wameandaa kwa mara ya kwanza wiki ya Uhasibu itakayofanyika jijini humo kuanzia Machi 9-14, 2020.

Wiki hiyo ya uhasibu itafanyikia viwanja vya Chuo kikuu Dar es Salaam na Kiwanja cha michezo cha Jakaya Kikwete kilichopo kidongo chekundu.

Mwambuja amesema lengo jingine la kufanya maadhimisho ni kutatua changamoto zilizopo kwa wahasibu wanaofanya kazi chini ya kiwango huku akitaja sababu mbili za kuwapo wahasibu wanaotoa huduma chini ya kiwango.

"Sababu ya kwanza unakuta mwanataaluma mwenyewe kutanguliza maslahi binafsi na kupotoka katika kuzingatia maadili ya umma, anafanya hivyo na sababu ya pili ni kubadilika kwa mambo katika taaluma hiyo kutokana na umuhimu wake," amesema Mwambuja

Mwambuja amesema mafunzo yatakayokuwapo katika wiki hiyo ambayo yatahudhuriwa na wanachama wakubwa mbalimbali akiwamo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovic Utouh na mawaziri wenye taaluma hiyo yatawasaidia kujua vitu vipya ili wasitoke nje ya taaluma na wataanzisha huduma mpya kuwapa mafunzo ya vitu vipya wanachama wote vinavyohusu taaluma hiyo.

Pia Soma

Advertisement

Katika maadhimisho haya ambayo wanatarajia watu zaidi ya 1,000 kuhudhuria kutakuwa na huduma mbalimbali za kijamii ikiwamo kuchangia damu, ushauri kwa wajasiriamali wanawake, kutoa ushauri wa kibiashara na kuwapa mahitaji wagonjwa.

Mwambuja amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya uhasibu ni 'mhasibu, mshirika katika kukuza uchumi wa viwanda na maendeleo ya jamii' na itawahusisha wahasibu wote kufika na kutoa huduma na kushiriki kongamano la biashara.

Naye Mkurugenzi wa Miradi na Mipango, Ezekiel Stephen amesema baada ya wiki ya uhasibu yote ambayo yanayofanyika kutakuwa na mwendelezo wake katika ofisi za uhasibu kupata elimu.

Katibu wa Wiki ya Uhasibu, Emilia Simon amewataka wanawake na watoto kujitokeza kwa wingi kupata huduma na elimu kuhusu uhasibu na biashara katika kuwasaidia kwenye shughuli zao za kila siku pia kwa wanafunzi wa kike ili kuongeza idadi ya wahasibu.

Chanzo: mwananchi.co.tz