Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wezi wa mifugo waundiwa mkakati Serengeti

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti.  Sasa ni kata baada ya kata ili kubaini watuhumiwa wa wizi wa mifugo katika wilaya ya Serengeti.

Leo Jumatatu Oktoba 7, 2019 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kisaka Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu  amesema lengo ni kubaini watuhumiwa ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

"Wananchi wanawafahamu watuhumiwa wa wizi na wamekuwa wakiwaficha huku lawama wakitupia serikali, sasa ni kata kwa kata kwa kuwashirikisha kupiga kura za siri ambazo kamati ya ulinzi inazifanyia kazi," amesema.

Amesema alianza na kata ya Manchira ,Morotonga na sasa Kisaka na kuwa hana ratiba maalum atakuwa anaenda anakoona inafaa kwa wakati huo.

Matukio ha wizi wa mifugo katika wilaya hiyo miaka  ya nyuma yalishamiri yakiambatana na matukio ya mauaji ,kwa sasa yameanza kushamiri katika maeneo mbalimbali ya wilaya.

Chanzo: mwananchi.co.tz