Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenyeviti 15 wajiuzulu Tarime

Waitara Chozi Pic Mwita Waitara

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeviti 15 wa vijiji na vitongoji kutoka Kata ya Kwihancha, Goronga na Nyanungu Tarime mkoani Mara, wamejiuzulu baada ya serikali kutoa msimamo wake juu ya wananchi kupisha maeneo ya hifadhi ya Serengeti kwa kuweka mipaka ambayo inatenganisha vijiji na hifadhi hiyo.

Hatua hiyo ya wenyeviti hao kujivua inakuja baada ya hivi karibuni Mawaziri wa kisekta waliotembelea eneo lenye mgogoro baina ya wananchi na hifadhi ya Taifa nakutoa msimamo wa serikali ndipo wenyeviti hao wakaamua kujivua uongozi.

Akizungumzia msimamo wa serikali Waziri wa TAMISEMI Angellah Kairuki, juu ya mipaka hiyo ambapo amesema walichokifanya ni kuweka vigingi imara na sio kubadili ramani iliyokuwepo tangu awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live