Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye ulemavu wamlilia Mkapa

Ca8729f8ba37a5b49eac9f6deba37bcf.png Wenye ulemavu wamlilia Mkapa

Thu, 30 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma (Chawata) kimesema Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alikuwa msaada mkubwa kwa watu wenye ulemavu ambapo katika awamu yake ya uongozi alianzisha mchakato wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ambayo ilitungwa mwaka 2004.

Akizungumza na HabariLEO jana, Katibu wa chama hicho mkoani Dodoma, Kalebi Muhawi alisema kifo hicho kimewahuzunisha kwani ameondoka akiwa bado anahitajika kutokana na kwamba katika kipindi cha uhai wake aliweza kufanya mambo mengi makubwa katika nchi ikiwemo kuitoa nchi katika hali mbaya ya uchumi na kuiweka katika hali nzuri.

Kalebi alisema katika upande wa elimu kwa watu wenye Ulemavu, Mkapa aliweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani changamoto zile ambazo walemavu walikuwa wakikumbana nazo wakati huo ikiwemo ya miundombinu, aliweza kuwasaidia kuondokana nayo.

Chanzo: habarileo.co.tz