Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye ulemavu wa ngozi waiomba Serikali kuwafanyia sensa

40029 PIC+SARATANI Wenye ulemavu wa ngozi waiomba Serikali kuwafanyia sensa

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Dar es Salaam. Watu wenye ulemavu wa ngozi wameiomba Serikali kufanya sensa kupata idadi yao kwa lengo la kuwahudumia kwa ufanisi ili kutokomeza vifo vinavyotokana na saratani ya ngozi.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Februari 4, 2019 na mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania, Nemes Temba wakati wa upimaji saratani kwa watu wenye ulemavu huo katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI).

Amesema kujulikana kwa idadi yao kutaiwezesha Serikali kutenga bajeti na kuwafikia watu wote kwa wakati na hivyo kutokomeza kabisa vifo vitokanavyo na maradhi ya saratani.

“Hii itasaidia pia kuwapatia bima za afya ili wapate matibabu sahihi kwa wakati sahihi, lakini pia tunaomba Serikali iendelee kuhakikisha bajeti ya mafuta kinga inatengwa na kuwa mafuta hayo yapatikane na kusambazwa kwa wote,” alisema Temba.

Hata hivyo, Temba amesema waraka wa matibabu bila malipo kwa watu wenye ulemavu bado ni tatanishi na husababisha wengi kushindwa kumudu gharama hasa matibabu ya saratani ya ngozi.

Mmoja wa waliofika kupima saratani, Christina Mathias amesema, “ Serikali itusaidie mafuta kinga wengi hatuna uwezo na kazi tunazofanya tunakuwa hatarini kupatwa na saratani ya ngozi.”

 



Chanzo: mwananchi.co.tz