Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye magari mabovu vijijini kukamatwa

Polisi Kamata Wenye magari mabovu vijijini kukamatwa

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP Solomon Mwangamilo amewataka madereva wanaofanya safari katika maeneo ya vijijini Mkoani humo kufanya matengenezo ya magari yao maarufu mando ili kuepusha ajali ambazo chanzo chake ni ubovu na kubeba watu kupita kiasi.

Ametoa kauli hiyo alipokutana na madereva katika Kijiji cha meserani Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha ambapo amewapa muda wa mwezi mmoja kufanya matengenezo ya vyombo hivyo na mara baada ya muda huo kuisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwa chombo amabacho kitabainika ni kibovu.

Aidha amesema kuna baadhi ya madereva wanao kiuka sheria za usalama barabarani kwa kubeba abilia hadi sehemu ya kuweka mizigo ambapo amesema kufanya hivyo ni kosa kisheria na inahatarisha Maisha ya binadamu ambapo amebainisha kuwa atakae fanya hivyo atakamatwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kata ya Meserani Bw. Loburu Moleli amesema wao kama viongozi wa jamii ya kifugaji watawaeleza maderva wa maeneo hayo kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali za mara kwa mara katika maeneo ya vijijini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live