Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye mabasi waomba spidi iongezwe

Mabasi Ms (5).jpeg Wenye mabasi waomba spidi iongezwe

Sun, 23 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) mkoani Mwanza kimetaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), kubadili ruksa ya spidi barabarani kutoka kilomita 80 kwa saa hadi 100 kutokana na maboresho makubwa yaliyopo barabarani.

Akizungumza na HabariLEO Katibu wa Taboa mkoani Mwanza, Anwar Said amesema barabara kwa sasa ni nzuri na pana hivyo kwa kuzingatia uwezo wa mashine za sasa ni vyema spidi ikabadilishwa na kuwa 100.

Aidha, amesema kuna haja ya kuweka vyombo vya kupunguza mwendo badala ya vinavyotumiwa kwa sasa ambavyo haviwezeshi kupunguza mwendo magari hayo bali humsaidia dereva kubaini kazi yake.

“Tunaomba tupate vidhibiti mwendo siyo vidhibiti dereva ili kuimarisha usalama kwa wasafiri wawapo safarini,” amesema Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live