Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye daladala watakiwa kuomba ‘ruti’ ya Mbezi Louis

5179014d54cc32c81cc55ed10ac5f851 Wenye daladala watakiwa kuomba ‘ruti’ ya Mbezi Louis

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka wenye mabasi ya daladala jijini Dar es Salaam, kuomba leseni ya njia ya Mbezi Louis, kuwarahisishia abiria wanaotumia Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kupata huduma kwa urahisi.

Kituo hicho cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi, kilizinduliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli, hatua iliyoondoa mabasi hayo katika Kituo cha Ubungo .

Akizungumza na HabariLeo jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara (LATRA), Johansen Kahatano alitaja njia ambazo hazijapata mabasi ni Mbagala hadi Mbezi na Bunju hadi Mbezi.

Alisema hadi kufikia hatua ya kuzinduliwa kwa kituo, tayari mabasi matano ya njia ya Mbagala hadi Mbezi yalikuwa yameomba kutoa huduma, lakini kwa njia ya Bungu hakuna.

“LATRA tunatoa mwito kwa wenye mabasi kuomba leseni za njia hiyo, tunajua kuwa suala hilo ni biashara lakini mikakati iliyopo ni kuhamasisha wenye mabasi kuweza kujitokeza ili kupunguza adha kwa abiria hao,” alisema.

Alisema mabasi mengi ya daladala yanafanya safari zake hadi kituo hicho, hivyo kwa maeneo ambayo hayajapata huduma, wananchi wanaweza kuonesha uhitaji ili wenye mabasi waweze kutoa huduma.

Wakati LATRA ikibainisha njia ambazo zina uhitaji mkubwa wa daladala zinazofanya safari kati ya kituo cha Mbezi Luis na maeneo mengine ili kuwezesha abiria waendao mikoani na nje kupata usafiri wa uhakika, kwa upande wa abiria wanaotumia kituo hicho wamekuwa wakilalamikia uchache wa magari katika njia zote.

Miongoni mwa abiria waliozungumza na gazeti hili ni wanaopanda daladala za Mbezi-Temeke, ambao waliiomba Latra kuangalia upya upangaji wa daladala katika njia tofauti kwa kuipa kila njia mabasi yake.

Chanzo: www.habarileo.co.tz