Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazungusha miiba ofisi ya kijiji, DC afika atoa maagizo

Miiba Miiba Wazungusha miiba ofisi ya kijiji, DC afika atoa maagizo

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Verified Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Kheri James @comradekheri , ameiongoza Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo kufika katika Kijiji cha Domanga ambacho hivi karibuni yalitokea mapigano baina ya Wananchi na kusababisha kujeruhiwa kwa Wananchi wawili ambapo Kamati hiyo imemaliza mgogoro huo.

Wakizungumza katika mkutano huo, Wananchi wa Kijiji hicho cha Damanga kilichopo Kata ya Hashkesh, Jimbo la Mbulu Vijijini wamesema kuwa chanzo cha mgogoro ni kuhisi kuwa zoezi la kudhibiti maeneo yaliozuiwa kwa malisho katika Kijiji hicho halisimamiwi kwa haki na usawa.

DC Kheri James ameagiza kufunguliwa kwa Ofisi ya Kijiji iliyokuwa imefungwa na kuzungushiwa miba na Wananchi wenye hasira kali na kisha amewasikiliza Wananchi wote wa Jamii ya Wahadzabe na Wadatogwa na kuwaeleza umuhimu wa kutumia vikao vyao vya Kijiji kujadili na kuamua mambo yao.

DC Kheri amewaeleza pia Wananchi hao madhara ya matumizi ya nguvu na uharibifu wa mali, kuwa vitendo hivyo havikubaliki na ni kinyume cha sheria.

Kamati ya usalama imezipatanisha pande zote mbili na imesistiza matumizi ya vikao vya kisheria kama njia ya kujadili na kuamua mambo yote yanayo husu Kijiji na Wananchi, pia Kamati imewatembelea Wananchi wawili waliojeruhiwa katika mapambano hayo ambapo hali zao kwa sasa zimeanza kuimarika na hali ya usalama katika Kijiji cha Domanga imerejea na Wanachi wameanza kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live