Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazoa taka waomba kukatiwa bima za afya

ZOAA TAKA Wazoa taka waomba kukatiwa bima za afya

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wazoa taka katika mkoa wa Dar es Salaam wameeleza namna wanavyodharaulika kwenye jamii kwa kutolewa lugha za kejeli huku wengine wakiiomba serikali kuwatambua kwa kukatiwa kadi za bima ya afya.

Akizungumza katika uzinduzi wa programu maalum ya wazoa taka, Mkurugenzi wa taasisi ya taka ni ajira Allen Kimambo, amesema wamekuja na programu hiyo ili waokota taka katika Jiji la Dar es Salaam waweze kupaza sauti zao ziweze kusikika kwa serikali na wananchi kutokana na kazi kubwa wanayoifanya kwenye jamii na kusababisha maeneo mengi ya jiji kuwa safi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija, amewataka wananchi wa wilaya hiyo na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla kutambua kwamba iwapo watashindwa kuweka mazingira yao kuwa safi basi watambue wanahatarisha usalama wa afya zao, ikiwepo kupata magonjwa ya mlipuko.

 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live