Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri avisimamisha vivuko viwili Mwanza

MV LINK Waziri avisimamisha vivuko viwili Mwanza

Mon, 14 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Serikali imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa vivuko viwili vya MV Athor na MV Orion vinavyofanya kazi kutoka Mwanza mjini kuelekea wilayani Sengerema mkoa Mwanza, baada ya kubainika kuwa na mapungufu, ambapo Waziri amesisitiza kuwa Wakuu wa mikoa na wilaya wasiingilie maamuzi hayo.

Submitted by Agnes Kibona on Jumamosi , 12th Jun , 2021 MV Orion, moja ya kivuko kati ya viwili vilivyosimamishwa kufanya kazi

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amesema kuwa zoezi hilo linaanza leo Juni 12, 2021, na kueleza kuwa awali vivuko vilipewa barua na Wakala wa Usafiri wa Majini (TASAC) ya kusitisha huduma za usafiri tangu Mei 25 mwaka huu kufuatia vivuko hivyo kubainika kutokuwa na cheti cha ubora, cheti cha usajili na cheti cha viwango na sifa za mabaharia.

Mbali na vyeti vyombo hivyo pia vilibainika kuwa na utata wa umiliki wa vyombo kwani wamiliki wa sasa walivinunua kutoka kwa mtu mwingine, pamoja na kupelekea kutopandishwa kwenye cherezo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuchunguzwa kama vinakidhi haja ya kuendelea kutoa huduma.  

Chanzo: eatv.tv