Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri atoa siku tano maeneo yanayokosa umeme Dar iwe historia

41658 Kalemanipic Waziri atoa siku tano maeneo yanayokosa umeme Dar iwe historia

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Nishati,  Dk Medard Kalemani ametoa siku tano kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kumaliza changamoto ya umeme kwenye maeneo yanayokosa nishati hiyo jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo ameeleza kuwa hana taarifa za kuwepo kwa mgao wa umeme, kutoa muda huo endapo kuna dosari zozote zitafutiwe ufunguzi.

Ametoa agizo hilo leo Jumatano Februari 13, 2019 alipotembelea kituo cha kufua umeme cha Kurasini kukagua utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya umeme jijini Dar es Salaam.

Dk Kalemani ameeleza kuwa kuna ziada ya umeme zaidi ya megawati 260, kushangazwa na taarifa kuwa umeme unakosekana.

“Katika siku hizo tano kama bado kuna eneo linakosa umeme naomba wananchi wanipe taarifa huyo meneja wa eneo husika aondolewe kazini maana itakuwa ameshindwa kazi,”



Chanzo: mwananchi.co.tz