WAZIRI wa Uvuvi na Mifugo, Mashimba Ndaki, amewataka watumishi wa kituo cha Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi (FRP), kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizopo katika kudhibiti uvuvi haramu na kutowaonea watu kwa kuwabambika kesi.
Waziri Ndaki ameyasema hayo katika ziara yake ya siku mbili mkoani Lindi baada ya kufika katika kituo hicho kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo.
“Nataka muwe waaminifu; hakikisheni faini zinazolipwa ziwe halali za kieletroniki badala ya kuwaandikia faini kwa risiti za mkono na kuwaonea wavuvi kwa namna yoyote,” amesema
Waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi yuko katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Lindi ambapo anatarajiwa pia kukutana na wakulima na wafugaji katika kuhakikisha serikali inaondoa kero za kutoelewana kati ya watu wanaojishugulisha katika sekta hizo mbili.