Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Deogratius Ndejembi ametoa rai kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuanza usanifu wa huduma hiyo kwa ajili ya majiji mengine makubwa likiwepo jiji la Dodoma
Ndembeji amesema kutokana na majukumu ya wakala huyo ni vyema kuanza mchakato wa kufanya usanifu wa huduma hiyo katika majiji makubwa likiwemo jiji la Dodoma.
“Rai yangu kwa DART ianze kuangalia maeneo mengine kama jiji la Dodoma, mfano kwa sasa TANROADS inaanza ujenzi wa njia nne kutoka Mji wa Serikali hadi katikati ya jiji, hivyo DART mzungumze na TARURA na TANROADS ili kwenye mipango yao waweze kuweka eneo la akiba katikati ya barabara”
Ameendelea kufafanua kua hatua ya kusanifu ikianza mapema itaondoa adha ya kuvunja vunja na kulipa fidia pindi upanuzi wa huduma hii utakapofika kwenye majiji makubwa.