Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri akita kambi kuzima moto Mlima Kilimanjaro

Moto Mlima Kilimanjaro T Waziri akita kambi kuzima moto Mlima Kilimanjaro

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, ameweka kambi katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikiwa ni mwendelezo wa ushiriki wake kuhakikisha moto unaowaka katika maeneo machache yaliyosalia katika hifadhi ya Mlima huo unazimwa.

Akiwa katika hifadhi hiyo Waziri Balozi Dkt. Chana amepokea taarifa ya utekelezaji wa kazi inayoendelea ya kuzima moto akiwashukuru na kuwapongeza wadau wote waliojitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha moto unadhibitiwa katika maeneo yote.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameendelea kukemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi wanaoanzisha au kuchoma moto hovyo katika maeneo yaliyohifadhiwa na kuisababishia serikali na wananchi wake hasara kubwa, na kusisitiza kuwa yeyote atakayebainika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live