Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri aagiza ng’ombe 179 waliokamatwa kwenye hifadhi kuachiwa

92122 Pic+kanyasu Waziri aagiza ng’ombe 179 waliokamatwa kwenye hifadhi kuachiwa

Fri, 17 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Constantine Kanyasu amewaagiza viongozi  wa Pori la Akiba  la Mkungunero kuwaachia ng'ombe 179 wa wafugaji wa kijiji cha Kimotorok.

Ng’ombe hao wa wananchi wa kijiji hicho kilichopo kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro mkoani Manyara walikamatwa Desemba 31, mwaka 2019.

Kanyasu ametoa agizo hilo jana Alhamisi Januari 16, 2020 baada ya wananchi hao kulalamika ng’ombe hao kukamatwa katika eneo ambalo Rais wa Tanzania, John Magufuli aliagiza wananchi waliopo hapo wasisumbuliwe.

Naibu waziri huyo amesema mifugo hiyo irudishwe kwa wafugaji,  kuwataka wahakikishe hawaingii katika pori hilo.

Amewataka wafugaji kuheshimu mipaka hadi Serikali itakapotoa tafsiri sahihi ya mipaka kumaliza migogoro ya wafugaji na hifadhi.

"Baadhi ya maeneo wafugaji waliingiza mifugo yao kwenye hifadhi ilikamatwa na kuuzwa, nyinyi mna bahati mnarudishiwa bila kutoa chochote nawaeleza hili na msirudie,” amesema Kanyasu.

Diwani wa Loiborsiret,  Ezekiel Lesenga amemshukuru naibu waziri huyo, kuimba Serikali kufanyia kazi kamati ya mawaziri wanane waliofika eneo hilo kutatua mgogoro wa mipaka.

"Wafugaji wanabughudhiwa kila mara na mifugo yao imekuwa ilikamatwa wakati inachungwa kwenye maeneo ambayo Rais  Magufuli aliruhusu," amesema.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimotorok, Eliya Parmelo amesema wanatambua kuwa Hifadhi ya Tarangire na Mkungunero ni mali ya Serikali na wananchi wote lakini isigeuke kuwa kero kwa jamii.

Chanzo: mwananchi.co.tz