Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy apiga marufuku walimu kukaimishwa kazi za maafisa kata na watendaji

Ummy Ummy.png Waziri wa Tamisemi ,Ummy Mwalimu akiwa Mkoa wa Pwani

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: Tamisemi

Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuwatumia waalimu kukaimu nafasi za utendaji wa vijiji, mitaa na kata bali waachwe wafanye kazi yao ya kufundisha hasa kutokana na upungufu uliopo wa walimu hapa nchini.

Akiongea na Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani leo Waziri Ummy amesema Wakurugenzi wamekuwa wakiwatumia Waalimu kukaimu nafasi ya utendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata suala hili halikubaliki kwa kuwa mwalimu ameajiriwa kwa lengo mahususi la kufundisha na sio kufanyakazi za utendaji wa kata, vijiji na Mitaa

“Kunachangamoto ya uhaba wa walimu nchini,hivyo tuwaache walimu wafanye kazi ya kufundisha, kwa kuwa jukumu kubwa la waalimu ni kufundisha, wasikaimishwe kwenye utendaji wa kata, mitaa na vijiji ” amesisitiza Waziri Ummy

Amesema kuwa Serikali inatambua ipo changamoto ya uhaba wa watendaji wa kata, vijiji na mitaa lakini amewataka Wakurugenzi kuanza kuwatumia watumishi wengine wa kada nyingine wakiwemo, maafisa maendeleo ya jamii ili kupunguza changamoto hiyo.

Aidha amezitaka Halmashauri zenye mapato kuajiri watumishi wa kujitolea kwa muda na pia kuhakikisha Mtendaji kukaimu mitaa miwili wakati halmashauri hizo zinajipanga. Aidha Wizara itawasiliana na Ofisi ya Rais Utumishi kuhusu kupata kibali cha kuajiri Watendaji wa Mitaa, Vijiji na Kata ili kupunguza upungufu uliopo.

Chanzo: Tamisemi