Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy amisimamisha kazi Mkurugenzi Sengerema

Ummy 1 0.jpeg Waziri Ummy amisimamisha kazi Mkurugenzi Sengerema

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Waziri wa Tamisemi,  Ummy  Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema,  Magesa Boniphace kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na kiitengo cha mawasiliano serikalini imeeleza kuwa Waziri Ummy amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo kutoka kwa wananchi na viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa Sengerema (CCM), Hamisi Tabasamu.

Katika taarifa hiyo, tuhuma hizo zimeelekezwa kwa mkurugenzi na baadhi ya wakuu wa idara za halmashauri hiyo zinaonyesha wanafanya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika halmashauri hiyo, na kuathiri utekelezaji wa miradi kwa kiwango kilichokusudiwa.

Kufuatia tuhuma hizo, Ummy amemuagiza katibu mkuu Tamisemi kuunda timu ya uchunguzi wa tuhuma hizo haraka.

Pia, amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha katika kipindi chote ambacho timu ya uchunguzi itakua ikifanya kazi katika halmashauri hiyo malipo yote yatakayofanyika kuanzia sasa yazingatie sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa fedha za umma.

“TUSIKAE KWA KUSUBIRIA MATAMKO, RIPOTI YA CAG IMEONESHA”— MBUNGE MATIKO

Chanzo: millardayo.com