Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy aagiza viongozi kuwa na lugha za staha

UMMY Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Ummy Mwalimu, amefanya kikao na Mbunge, Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema akiwataka viongozi hao kufanya kazi kwa kushirikiana na kuaminiana pamoja na kutumia lugha za Staha wakati wanapokosoana.

Hatua hii inafuata baada ya Waziri Ummy, kugundua changamoto za kiutendaji katika wilaya hiyo hali iliyopelekea kuzorota kwa miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.

"Ninyi ndio Engine ya Halmashauri mnapaswa kusimamia ukusanyaji wa mapato ipasavyo na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato huku mkihakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unafanyika kwa ufanisi"

Waziri Ummy,alitembelea baadhi ya Shule katika Halmashauri hiyo na kugundua kuwa bado wanafunzi wanakaa chini kwenye vumbi kutokana na ukosefu wa madawati, hivyo amewataka tena hii leo Agosti 17,2021, viongozi hao kushirikiana kutatua changamoto hizo kwa umoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live