Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ndalichako aagiza mhandisi, mshauri elekezi ujenzi wa Veta kukamatwa

90946 Pic+ndalichako Waziri Ndalichako aagiza mhandisi, mshauri elekezi ujenzi wa Veta kukamatwa

Mon, 6 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sumbawanga. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani mhandisi na mshauri elekezi wa mradi ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mhandisi huyo ni Dingi Fubing raia wa China na mshauri elekezi, Swalehe Kyabega ambaye ni Mtanzania.

Wataalamu hao wa ujenzi wanadaiwa kushindwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa chuo hicho huku wakitoa taarifa zisizo sahihi kwa Profesa Ndalichako ambaye leo Jumatatu Januari 6, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho unasuasua.

Ujenzi wa chuo hicho ulioanza Julai 31, 2018 ulitakiwa kukamilika Septemba 2019. Baada ya muda huo kufika mkandarasi aliongezewa siku 100 ambazo nazo ziliishia pasina kumaliza kazi hiyo.

Baada ya kutoa maagizo hayo, polisi waliokuwapo eneo hilo waliwakamata na kuwabeba kwenye gari lao na kuondoka nao kwenda mahabusu ya kituo kikuu cha kati Sumbawanga mjini.

Profesa Ndalichako amewataka polisi kutowaachia watuhumiwa hao lakini amewaruhusu kuendelea kufanya mawasiliano na wenzao ili kukamilisha ujenzi huo ambao hata hivyo waziri huyo hakutoa muda rasmi.

Profesa Ndalichako ameendelea na ziara wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa nchini Tanzania.

Chanzo: mwananchi.co.tz