Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu awaonya viongozi Kibondo

42585 Waziripic.png Waziri Mkuu awaonya viongozi Kibondo

Tue, 19 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibondo. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kibondo kuacha tofauti baina yao zinazosababisha washindwe kufanya shughuli za maendeleo.

Mbali na kauli hiyo, Majaliwa amemsimamisha kazi mhasibu mkuu wa halmashauri ya Kibondo, Thomas Chongoro kutokana na sintofahamu katika ukusanyaji wa mapato.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 19, 2019 katika kikao cha

watumishi, akibainisha kuwa wamekuwa wakiishi katika makundi akiwataka waache tabia hiyo kabla hawajawajibishwa.

Amebainisha kuwa kazi ya watumishi ni kuwatumikia wananchi, akibainisha kuwa Serikali inatoa fedha nyingi katika miradi mbalimbali katika halmashauri lakini makusanyo ya ndani hayaridhishi.

“Lazima wananchi waone mabadiliko kwa sababu Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Ukiangalia mwaka wa fedha 2018 /19 mmekusanya asilimia 29 ambayo haifiki hata robo ya makusanyo ya kiwango cha chini walichowekewa cha asilimia 80, “ amesema Majaliwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz