Sun, 6 Nov 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewajulia hali waathirika wa ajali ya Ndege ya Precision Air wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera iliyotokea mapema leo asubuhi.
Awali Waziri mkuu Majaliwa alipata wasaa wa kuzungumza na umati wa wananchi na viongozi waliokuwepo katika eneo hilo na kusema Rais Samia Suluhu Hassan anatoa pole kwa wote walioguswa na ajali hilo na kwamba Serikali itaendelea kutoa huduma stahiki kwa majeruhi wote.
Pia, amewataka wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ambacho Serikali itafanya uchunguzi kupitia vyombo vyake ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live