Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu ampa miezi 2 Mkurugenzi Lindi kujenga kituo cha magari makubwa

MIZANI 67 Waziri Mkuu ampa miezi 2 Mkurugenzi Lindi kujenga kituo cha magari makubwa

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa muda wa miezi miwili kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi kujenga kituo cha mabasi na malori katika eneo la Mnazi Mmoja, ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo.

Ametoa muda huo mara baada ya kukagua mizani katika eneo la Mnazi Mmoja lililopo manispaa ya Lindi.

Amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Lindi kujenga mizani nyingine katika eneo la Mnazi Mmoja kwa kuwa mji huo unakuwa kwa kasi na idadi ya magari inaongezeka.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, tayari Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mizani hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live