Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Majaliwa kuzindua Daftari la Mpiga kura Moshi Julai 18

65837 Majaliwa+pic

Sun, 7 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Wananchi Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli ya uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la Wapigakura, inayotarajiwa kufanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Julai 18,2019.

Wito huo umetolewa leo Jumamosi, Julai 6, 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge na Watu wenye ulemavu wa Tanzania, Jenista Mhagama, wakati alipotembelea Uwanja wa Mandela, uliopo Kata ya Bomambuzi Mjini Moshi.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi tayari imemaliza maandalizi yake ya uboreshaji wa Daftari la Mpiga kura, kwa mujibu wa sheria, na Julai 18, Waziri Mkuu, atafika Moshi viwanja vya Mandela kuzindua uboreshaji huo, niwaombe wananchi, wajitokeze kushirikiana na Waziri Mkuu,” alisema  Mhagama.

Waziri Mhagama alisema utaratibu huo ni wa kawaida na sheria inataka Tume ya Uchaguzi kama sehemu ya majukumu yake kuboresha Daftari la Mpiga kura na kwamba, uboreshaji huo baada ya kuzinduliwa utaanzia katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage alisema watakaoandikishwa na kuingizwa katika Daftari hilo ni wale ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha mwaka 2015 na wale ambao hawakuwahi kujiandikisha.

“Hatutawaandikisha wale ambao waliwahi kuandikishwa hapo awali, safari hii zoezi la uandikishaji litawahusu, wale ambao wameshafikisha umri wa miaka 18 ya kuzaliwa na wale ambao watataka kubadilisha taarifa zao, ama wale wamehama maeneo waliyokuwa wakiishi awali na kuwaondoa kwenye daftari wale waliofariki,”, alisema.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz