Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mbarawa atoa sababu za maji kuadimika Njombe

51807 Maji+pic

Thu, 11 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema uhaba wa maji katika mji wa Makambako mkoani Njombe unatokana na ongezeko kubwa la watu.

Amesema mbali na ongezeko la watu, uhaba huo unachangiwa na uchakavu wa miundombinu iliyojengwa tangu mwaka 1980.

Akizungumza wakati wa ziara ya Rais John Magufuli mkoani Njombe leo Alhamisi Aprili 11, 2019 Profesa Mbarawa amesema upatikanaji maji kwa sasa ni asilimia 61.2 licha ya mkoa huo kuzungukwa na vyanzo vya maji ikiwamo mito.

Profesa Mbarawa ameeleza kuwa ipo mipango mbalimbali na Serikali itatatua tatizo hilo litaisha na kubaki historia.

 “Tuna mipango ya aina mbili; wa kwanza ni ule unaoendelea wa kutoa maji kwenye chanzo cha bwawani uliofikia asilimia 60 umeanza kutoa maji,” amesisitiza kiongozi huyo.

Amesema mradi wa pili utakaohudumia miji 28 ya Tanzania umepatikana kupitia mkopo wa masharti nafuu wa Sh1 trilioni kutoka nchini India.

“Leo naahidi tena kwamba tupo kwenye utaratibu wa kupata mtaalamu mshauri ikifika Septemba mtaalamu atakuwa ameanza ujenzi,” amesisitiza.

Kuhusu upande wa vijijini, Profesa Mbarawa amesema Sh15.9 bilioni zinatumika katika miradi mitano ya maji katika vijiji vya mkoa huo.

“Niwaahidi wakazi wa mkoa wa Njombe kwamba tatizo la maji litakuwa historia,” amesisitiza.



Chanzo: mwananchi.co.tz