Arusha. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Stella Manyanya amewatembelea wafanyakazi wa kampuni ya Azam Media, Artus Massawe na Mohammed Mahinde wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Selian jijini Arusha.
Wafanyakazi hao walikuwa katika gari aina ya Toyota Coaster lililopata ajali Julai 8, 2019 na kusababisha vifo vya wafanyakazi watano wa kampuni hiyo na madereva wawili wa gari hilo lililogongana uso kwa uso na lori.
Wafanyakazi hao walikuwa wakielekea wilayani Chato mkoani Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato.
Akizungumza leo Alhamisi Julai 11, 2019 mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk Paul Kisanga amemueleza Manyanya kuwa hali za wafanyakazi hao ni nzuri.
Kisanga amesema baada ya jana kufanyiwa upasuaji na dawa wanazotumia wanaona mabadiliko yanayowapa matumaini.
Kwa upande wake Manyanya ameridhishwa na hali zao kuwaombea wapone haraka ili waendelee kulitumikia Taifa kupitia tasnia ya habari.
Pia Soma
- Boti za Iran zajaribu kuikamata meli ya mafuta ya Uingereza
- Askari adai wanafunzi walikiri kusambaza picha za Magufuli akiwa amevaa Hijab
- Rais Magufuli ampigia simu waziri Mbarawa mkutanoni, ampa maagizo
Daktari wa upasuaji katika hospitali hiyo, Peter Makanza amesema Mahinde amefanyiwa upasuaji mara tatu na hali yake ikiimarika atafanyiwa upasuaji mwingine.