Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Lukuvi atua Mara kutekeleza agizo la JPM

17735 Pic+lukuvi TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameanza ziara mkoani Mara.

Akiwa mkoani Mara pamoja na mambo mengine Lukuvi anatarajiwa kutatua migogoro ya ardhi kama alivyoagizwa na Rais John Magufuli alipofanya ziara mkoani humu hivi karibuni.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na wizara ya Ardhi akiwa mkoani Mara Waziri Lukuvi anatarajiwa kukutana na wananchi mbalimbali akiwemo bibi Nyasasi Masige mkazi wa wilaya ya Bunda aliyetoa malalamiko yake mbele ya Rais juu ya kuporwa ardhi yake.

Bibi huyo alimwambia Rais Magufuli licha ya kuporwa ardhi alijitahidi kutafuta haki yake bila mafanikio hali iliyosababisha Rais Magufuli kumpigia simu Waziri Lukuvi kutaka kujua namna suala la bibi huyo lilivyoshughulikiwa kabla ya kumtaka waziri huyo kumsimamisha kazi kamishna wa ardhi Kanda ya Simiyu kwa kushindwa kusimamia haki ya bibi huyo.

Mbali na bibi huyo ambaye atatembelewa leo Septemba 17, 2018 Waziri Lukuvi anatarajiwa kuwatembelea mabibi wengine wawili katika manispaa ya Musoma ambao hata hivyo majina yao hayajapatikana kwa ajili ya kukagua viwanja vyao wanavyodai kuwa wameporwa.

Pia, waziri huyo atakutana na wananchi 37 wa manispaa ya Musoma ambao kupitia programu ya funguka na waziri Lukuvi waliwasilisha kero zao za ardhi kabla.

Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi anatarajiwa kutembelea wilaya za Bunda, Musoma na Tarime.

Akiwa mkoani Mara Rais Magufuli aliagiza uongozi mkoani Mara pamoja na wizara mbalimbali kushughulikia kero za wananchi huku akisema mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa yenye kero na  migogoro mingi ya wananchi ikiwemo migogoro mingi ya ardhi.

Chanzo: mwananchi.co.tz