Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Lukuvi apongezwa kuwa mwanafunzi bora

78364 Lukuvi+piv

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi amepongezwa kwa kukitangaza vema Chuo cha Ualimu Tabora kwa vile ni tunda lake.

Akimzungumzia waziri huyo leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 katika Jubilee ya miaka 50 ya chuo hicho, Mkuu wa chuo hicho, Sista Agnes Awaki amesema Lukuvi alikuwa mwanachuo aliyeingia mwaka 1968 na kumaliza 1969 akisomea astashahada ya Ualimu.

Ameeleza Waziri Lukuvi pia alikuwa miongoni mwa wanachuo waliosoma wakati chuo kikitoa mafunzo ya Kijeshi kuanzia mwaka  1975 hadi 1992 yalipositishwa.

Sista Agnes amesema wanajifunza kutoka kwake kujiendeleza na kuchapa kazi kwa umahiri na umakini mkubwa kwa kutoa mfano wa utendaji wake wa kazi kuwa unawabeba wao kama chuo.

"Tunatembea kifua mbele kutokana na uchapakazi wako mkubwa ukiwa ni zao la chuo chetu," amesema

Amewataka wanachuo na wahitimu wa chuo hicho, kuiga mazuri yote yanayofanywa na waziri huyo ambaye wanamchukulia kama kiongozi aliyetukuka.

Pia Soma

Advertisement
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema waziri huyo amedhihirisha kuwa chuo hicho kinatoa watu mahiri wenye weledi ambao wana uwezo mkubwa wa kuongoza.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz