Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Jafo awaondoa hofu Watanzania

70234 Jafo+pic

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) nchini Tanzania, Selemani Jafo amewaondoa hofu Watanzania kuwa kukamilika kwa hospitali mpya 67 na vituo vya Afya 352 katika wilaya zote nchini, kutakwenda sambamba na uhakika wa wataalamu wa Afya pamoja na vifaa tiba.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Agosti 6, 2019 Wilayani Mvomero baada ya kutembelea na kukagua hospitali ya wilaya hiyo, ili kuangalia hali halisi ya ukamilishaji wa hospitali za wilaya.

Aidha, waziri huyo licha ya kuridhishwa na ukamilishaji wa ujenzi kwa asilimia 99 nchi nzima, amesema bado maeneo machache yakiwamo ya Malinyi, Morogoro vijijini na Mtwara vijijini, zimeshindwa kufikia malengo yaliyowekwa.

 

Waziri Jafo ameahidi hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu, majengo yote yatakuwa yamekamilika na kwamba atakutana na wakuu wa mikoa kwa lengo la kuweka mikakati zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe akizungumza katika ziara hiyo, amemwambia Waziri kuwa kukwama kwa ujenzi wa baadhi ya hospitali mkoani kwake kunatokana na uzembe na jiografia kwa maeneo yaliyojengwa hospitali kuwa mbaya.

Pia Soma

Dk Kebwe amesema kama mkoa, wanaendelea kusimamia kikamilifu ili ujenzi huo ili ukamilike kwa  wakati na hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa na Serikali kwa wilaya ambazo zinasuasua kama ya Morogoro

Katika siku za hivi karibuni, Waziri Jafo aliagiza ifikapo Julai 30, mwaka huu, ujenzi huo uwe umekamilika na aliwataka wakurugenzi, wakuu wa wilaya na mikoa kusimamia kwa karibu ujenzi huo.

Naye mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly amesema kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hizo wilayani kwake kumechangiwa na ushirikiano kutoka kwa wananchi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz