Arusha. Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Innocent Bashungwa amevitaka viwanda vya A to Z na Sunflag vilovyopo jijini Arusha kutengeneza vifungashio vya bidhaa za wajasiriamali wadogo ili kuwasaidia kupata masoko na kukuza biashara zao.
Akizungumza baada ya kutembelea viwanda hivyo jana Jumapili Julai 21,2019, Waziri Bashungwa alisema wafanyabiashara wadogo wanauhitaji mkubwa wa vifungashio vya bidhaa zao.
"Katika bidhaa ambazo mnatengeneza mnaweza pia kutengeneza vifungashio vya wajasiriamali wadogo kwani kuna uhitaji mkubwa" alisema.
Hata hivyo, waziri huyo alieleza kuridhishwa na utendaji wa viwanda hivyo ambavyo vimesaidia kutoa ajira kwa vijana wengi katika jiji la Arusha.
Mkurugenzi wa kiwanda cha A to Z, Jayant Shah alisema wanaunga mkono wazo la waziri huyo kwa kufanya jitihada ya kutengeneza vifungashio vitakavyokidhi mahitaji ya wafanya biashara wadogo.
"Niwazo zuri ambalo waziri amelitoa tuko tayari kulifanyia kazi," alisema
Pia Soma
- Jaji Kiongozi Tanzania atoa maagizo kwa majaji, mahakimu
- Mwinyi atamani shule ya Ahmes ishike nafasi ya kwanza kabla hajafa
- Alichokisema Lugola baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za magereza
Mahundi aliomba pia Serikali kulegeza masharti kwa wataalamu kutoka nje ili waje nchini jambo linalosaidia kuongeza ujuzi kwa Watanzania.
Viwanda vya A to Z na Sunflag ni viwanda vya muda mrefu mkoani Arusha vikijihusisha na utengenezaji wa nguo, vyandarua, nyavu za uvuvi na bidhaa nyingine mbalimbali.