Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Aweso aomba radhi

Aweso Azungumzia Upungufu Wa Maji Mwanza Waziri Aweso aomba radhi

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefika katika Kijiji cha Uhambingeto, Wilayani Kilolo na kuwaomba radhi wananchi wa kuchelewa kukamilika kwa mradi wa maji.

Licha ya kununua dumu moja ya kunywa kati ya Sh2000 hadi 5000, wananchi hao wamekuwa wakitumia maji ya bwawa ambayo pia hutumika kunywesha mifugo.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo alimuagiza wazir huyo kufika kijijini hapo na kuwaomba radhi wananchi kwa kukwama kwa mradi huo unaogharimu zaidi ya Sh2.1 bilioni.

Mbali na kutaka Aweso afike, aliagiza mradi huo ukamilike Septemba mwaka huu na wananchi wanze kupata maji.

Aweso ambaye alipokelewa na wimbo wa kihehe 'Twasindilige yi veve' ikimaanisha tulikuwa tunakusubiri wewe aliahidi kuwa mradi uliokwama kwa zaidi ya miaka kumi utakamilika ndani ya miezi mitatu.

"Nawaomba radhi wananchi wa Uhambingeto na viongozi wote wa Wilaya na Mkoa, hatutaongeza siku wala sijui dizaini imefanyaje hayo mambo ni ya kwetu, na kuanzia kesho kazi ya vituo vya maji itaanza," amesema Aweso na kuongeza;

"Kama wangekuwa hawana fedha tungesema changamoto ni fedha lakini wanazo, zitoke zitumike kwa ajili ya mradi huu."

Skimu ya Ruaha Mbuyuni

Katika Skimu ya Umwagiliaji ya Ruaha Mbuyuni ambayo imebomoka na kusababisha maji yahame, Aweso ameahidi kuanza kuifanyia kazi haraka.

"Tunao wataalamu wengi watakuja na hapa tutaweka tuta, hatutategemea wakandarasi," amesema Aweso.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga amesema miradi hiyo ilikuwa kati ya Ile inayomuumiza kichwa kwenye jimbo lake.

"Miradi hii ikikamilika ndani ya muda mfupi itawafanya wananchi waendelee kuiamini CCM, binafsi nashukuru kwa hatua hii kubwa," amesema Nyamoga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live