Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Aweso afyeka vigogo wa Maji Karatu

1dd91b274c214031987dfd20d38c32bf.png Waziri Aweso afyeka vigogo wa Maji Karatu

Tue, 1 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA).

Waziri Aweso amefikia uamuzi huo, baada ya kufuatilia na kubaini ubadhilifu mkubwa sekta ya maji, ambapo amebaini bei ya maji ni kubwa na upangaji wake umekosa vielelezo muhimu.

Hatua hiyo imekuja baada ya kufanya ziara maalumu ya kikazi mjini Karatu jana, na kupokea taarifa ya utoaji wa huduma ya maji katika mji huo.

Pia Aweso ameahidi wakazi wa Karatu kuwa serikali inafanya mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma ya maji, kufuatia ukaguzi alioufanya katika ofisi za KARUWASA na kusisitiza kutekeleza mageuzi makubwa ya utendaji katika mamlaka hiyo.

Amesema kiasi cha Sh bilioni 4, zitaelekezwa mjini Karatu, ili kuboresha miundombinu ya maji katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa bei rafiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live