Tue, 11 Jul 2023
Chanzo: Jamii
Baadhi ya Wazee wenye Ugonjwa wa Busha Wilayani Pangani, wamesema hawako tayari kutibiwa na wako tayari Kufa kuliko kuhudumiwa na Watoa Huduma wa Kike.
Wamemuomba Mkuu wa Wilaya, Zainab Abdallah, awapatie Watoa huduma wa Kiume
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja kati ya Wazee hao amesema licha ya Serikali kutoa Matibabu, wengi wao wamekuwa wakitoroka Hospitali muda wa upasuaji kutokana na kuandaliwa na Watoa Huduma wa Kike huku wengine wakiwa wadogo kiumri
DC Zainab amemuomba Mganga Mkuu wa Wilaya kufanyia kazi malalamiko ya Wazee hao
Chanzo: Jamii