Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee, machifu wajadili uharibifu wa mazingira Same

Wazee Pic Data3 Wazee na Machifu wa jamii za Same wakiwa kikaoni

Thu, 17 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Wazee wilayani Same Mkoani Kilimanjaro (Juwasa) na umoja wa machifu wamekutana kujadili hatma ya maendeleo na utunzaji wa mazingira ndani ya Wilaya hiyo.

Katika mkutano huo wazee ambao wazee hao waliwahusisha machifu saba wa kipare, wamejadili namna ya kuboresha mazingira na kukemea vitendo vinavyoharibu mazingira katika wilaya hiyo.

Miongoni mwa vitendo walivyojadili katika kikao hicho ni pamoja na ukataji miti kiholela, kurudisha maeneo ya misitu ya asili sambamba na uchomaji moto kwenye misitu.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 17, 2022 wakati wa kikao cha pamoja, Mwenyekiti wa Juwasa, Deoglas Msangi amesema kumekuwapo na uharibifu wa mazingira na miundombinu ya umwagiliaji katika wilaya hiyo jambo ambalo linahatarisha mazingira na maendeleo ya wilaya hiyo kwa ujumla.

Msangi amesema kabla ya uhuru na miaka michache baada ya uhuru utawala wa machifu ulikuwa na mafanikio makubwa kimaendeleo hasa katika utunzaji mazingira lakini baada ya kuondolewa kwa utawala huo vitu mbalimbali vya asili na kimila vilianza kutoweka ambapo amedai kuwa hali hiyo inaathiri kizazi cha sasa.

"Tumeona baada ya miaka kumi ijayo wapo watu watakufa njaa kama hatutaamua kuweka makubaliano ya pamoja na kuaanza utekelezaji wa kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, kufufua malambo ya mifugo ambavyo vyote hivi vilikuwapo enzi za nyuma na vilisaidia sana jamii yetu machifu ni watu ambao wako karibu na wananchi kule vijijini na wanataratibu zao za kusimamia maeneo yao tumeamua kukaa pamoja nao tuelezane ukweli ili kunusuru jamii yetu"

Advertisement "Ukiangalia maeneo mengi ile misitu ya asili ilikuwapo zamani ambayo ilikuwa chachu kubwa ya mvua sasa hivi misitu hiyo mingi imetoweka unaweza kushangaa hata kwanini mvua imekuwa ya kusuasua hivi, ni kwasababu ya kuharibu mazingira hivyo yote haya tumeadhimia kuyarudisha kwenye jamii yetu ya Wapare wa Same” amesema Msangi"

Mwenyekiti wa machifu wa Wilaya Same ambaye pia ni chifu wa Suji, Reuben Mashika amesema kupitia kikao hicho sasa wanaenda kuanza upya usimamizi wa maendeleo ndani ya Wilaya hiyo kwa kuhakikisha yale yote yaliyokuwa yameasisiwa na wazee wa zamani kwa lengo la maendeleo yanafufuliwa na kuwanufaisha wananchi.

Walezi wa Jumuiya hiyo ya wazee wilayani Same akiwamo Askofu mstaafu Jimbo Katoliki la Same, Jacob Koda na Mchungaji mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Same, Silvanus Mshana wamesema uumbaji wa Mungu wakati anaiumba Dunia ulienda sambamba na mazingira ambayo yalikuwa chachu kubwa kwa binadamu wa kwanza hivyo wamehimiza upandaji miti na utunzaji wa misitu ili kuyanusuru mazingira katika Wilaya hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live