Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee acheni kuoa mabinti

0f66f2d04f02b7cd9cb1ce94ad149d80 Wazee acheni kuoa mabinti

Wed, 30 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BARAZA la Wazee Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya limewasihi wazee kuacha tamaa ya kuoa mabinti baada ya wake zao kuzeeka kwa kuwa kufanya hivyo wanahatarisha maisha kutokana na maradhi ukiwemo upungufu wa kinga mwilini (Ukimwi).

Katibu wa Baraza la Wazee Wilaya ya Mbarali, Hezron Kapwela ametoa ushauri huo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika kikata katika Kijiji cha Azimio Mswiswi Kata ya Kongolo wilayani Mbarali.

Kapwela alisema kumekuwa na tabia ya wazee kuongeza mke baada ya wake zao wa awali kuzeeka au kufariki dunia.

“Ukiangalia picha za ujana wako utaona ulikuwa na nywele zote nyeusi tiii...lakini leo hii ukijiangalia kwenye kioo utaona kichwa chote ni kama kimemwagiwa unga.

Chanzo: habarileo.co.tz