Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee Tanzania waiangukia Serikali

Wazee Tanzania waiangukia Serikali

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Uvinza.  Baadhi ya wazee wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania wameiomba Serikali kuitungia sheria na sera ya taifa ya wazee ya Septemba 2003 ili waweze kuthaminiwa na kusaidia halmashauri zote nchini humo kwa mamlaka kutenga bajeti kwaajili ya kundi la wazee.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 26, 2019 katika kikao cha uhusishwaji wa maswala ya wazee katika mipango na bajeti za serikali, kilichoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Saidia Wazee Tanzania (Sawata), kwa kushirikiana na HelpAge International Tanzania, kilichofanyika wilayani humo, Katibu wa baraza la wazee mkoa wa Shinyanga, Anderson Lyimo amesema wazee ni kundi  limesahaulika katika jamii.

Amesema tatizo kubwa ambalo linasababisha mabaraza ya wazee Tanzania yasiingie kwenye bajeti za halmashauri za wilaya ni kwa sababu sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 hadi sasa haijatungiwa sheria.

Katibu Mkuu wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee Tanzania, Livingstone Byekwaso amesema wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo kuwa na  kipato duni huku taasisi nyingi za kifedha zimeshindwa kuwakopesha na kuwalenga zaidi kundi la vijana na wanawake.

Mwenyekiti wa Sawata wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Paulo Chabande amesema lengo la kuwakusanya kwa pamoja baadhi ya wazee wa wilayani hapo ni kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kujua haki zako kama kundi la wazee.

Kaimu Ustawi wa Jamii wa wilaya ya Uvinza, Priska Mhando amesema katika kupanga bajeti katika halmashauri hiyo watahakikisha wazee wanapata huduma zao za msingi ikiwamo huduma za afya, wanathaminiwa na kuhakikisha wanashirikishwa katika mipango mbalimbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz