Wazee kijiji cha Kwamsisi wilayani Handeni mkoani Tanga wamezuia ujenzi wa barabara ya lami ya Afrika Mashariki inayopita katika kijiji hicho mpaka watakapopatiwa shilingi milioni 15 kwa madai wanataka kutambikia barabara hiyo kabla ya ujenzi haujaanza.
Barabara hiyo ambayo inatokea jijini Tanga kupitia Pangani na kuingia kijijini hapo imelazimika kusimama kufuatia madai ya wazee hao ambao wanadai nia yao ni njema.
Wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Bi. sideli nchembe kujadili suaa hilo ambalo limesababisha mkandarasi kusimamisha ujenzi huo.
wazee hao wamesema kuwa;
"ilikuwa ni milioni 15 tumeupunguza kila kitu ili tufanye tambiko shida hapa ni pesa, tambiko la kwanza limeshafanyika ili waanze ujenzi kwa usalama" Amesema mmoja wa wazee hao
"tunataka kufanya tambiko ili kupooza miti itakayo katwa hapa, lakini pia hili suala lina athiri mfumo wetu wa maisha hapa tutakosa aji hivyo watulipe fedha hizo"
Sakata hilo limepokelewa tofauti na wananchi wa kijiji hicho ambao wengi ni wakulima wa zao la muhogo, na mara nyingi wanashindwa kusafirisha mazao yao kwa ubovu wa barabara, wamelaani vikali kauli za wazee hao,
"Mate ya milioni 15 uliyaona wapi!, hii barabara tunaihitaji sana, kinachoendela sasa si sawa", amesema mwanakijiji
"Barabara hii ilikuwa isipite hapa kuipata ni neema hivyo tusifanye kuweka vikwazo vingi" ameongeza mzee mmoja.
Nae Mkuu wa Wilaya hiyo ametoa muda wa siku tatu kwa wanakijiji hao kukubaliana kwani wakandarasi wapo tayari kulipa fidia hiyo, na amewataka wakandarasi hao kuhakikisha kuwa ujenzi huo hautaathiri vyanzo vya maji kijijini hapo