Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazee Chato kumuunga mkono Rais Samia

8e9c4cdbde62b70a4b6ea72e8d580df4.jpeg Wazee Chato kumuunga mkono Rais Samia

Sat, 27 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UMOJA wa Wazee Wilaya ya Chato mkoani Geita umemhakikishia kumuunga mkono Rais Samia Suluhu kama ilivyokuwa kwa Dk Magufuli ili aweze kukamilisha miradi iliyokuwa imeahidiwa na kupangwa na mtangulizi wake.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wilayani humo, Samwel Bigambo alisema hayo akitoa salamu za rambirambi. Alisisitiza kuwa wazee wa Chato wana imani na Samia kwani amefanya kazi akiwa msaidizi wa Magufuli.

“Kwa uzoefu wangu mara zote huwa wanasema, bora atangulie kufa baba kuliko mama, na kina mama wanaweza, kina mama huwa hawashindwi kitu, tunaamini mama yetu Samia ataendeleza yote yaliyofanywa na kijana wetu ambaye ametangulia mbele za haki,” alisema Bigambo.

Alisema wazee watamkumbuka zaidi Magufuli kwa jinsi alivyoweza kuthamini nafasi ya wazee nchini kwa kusisitiza kipaumbele cha wazee katika huduma za kiofisi na kijamii hasa za afya.

Bigambo alishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli kwa kurejesha umoja na mshikamano kwa watanzania wa dini zote. Alimuomba Rais Samia kuendeleza hayo ili Tanzania ibakie kuwa nchi yenye uhuru wa kuabudu kwa waumini wa dini zote.

Chanzo: www.habarileo.co.tz