Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazazi wawakomalia wanafunzi shule ya msingi Airport mkoani Kigoma

Thu, 22 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Kutokana na matokeo mabovu ya mitihani ya kujipima nguvu kwa wanafunzi wa darasa la saba halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji, wazazi wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Msingi Airport wameanza mikakati kukuza uelewa kwa watoto wao.

Wakizungumza katika kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo leo Jumatano Agosti 21, 2019 mwalimu mkuu wa shule hiyo, Sabas Rugai ametaja utoro kuwa sababu mojawapo inayofanya wanafunzi kufeli masomo.

Amesema katika mtihani huo uliofanyika Agosti 2019, wanafunzi 70 ndio walipata daraja C kati ya wanafunzi 192 wa darasa la saba shuleni hapo.

Wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo ya ziada jioni na utoro kwa baadhi ya yao unatajwa kuwa sababu ya kufeli, ikiwa ni muda mfupi kabla ya kufanya mtihani wa Taifa kuhitimu elimu ya msingi.

Mwenyekiti wa kamati ya shule, Jackson Sabuwanka ameomba wazazi kuendelea kushirikiana na walimu ili iwe rahisi kubaini changamoto zinazochangia wanafunzi kufanya vibaya katika mitihani yao.

Mwaka 2018 shule hiyo ilikuwa kati ya shule 10  zilizofanya vibaya kati ya shule 45 za manispaa ya Kigoma Ujiji.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz