Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazazi watakiwa kuwalea watoto katika maadili

Mon, 16 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wazazi nchini Tanzania wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili ili waweze kuwaheshimu walimu wanapokuwa shuleni jambo litakalowasaidia kufanya vyema katika masomo yao.

Hayo yameelezwa jana Ijumaa Septemba 13, 2019 na mdhibiti ubora wa shule kanda ya Dar es Salaam, Erick Ngoda katika mahafali ya 11 ya wanafunzi  wa darasa la saba Shule ya  awali na Msingi ya Montain Hill iliyopo Kimara, Dar es Salaam.

Ngoda amesema watoto wanahitaji kulelewa zaidi katika maadili mema wakiwa nyumbani, ikiwa kinyume chake wakifika shuleni hawawaheshimu walimu na kufanya vibaya katika masomo.

"Wazazi wakiwa na nidhamu watoto wao watakuwa na nidhamu wakija shuleni watawaheshimu na watakuwa wasikivu,  wanapokuwa darasani lazima watafanya vizuri katika masomo yao," amesema Ngoda.

Mkuu wa Shule hiyo, Gasper Shayo amesema wanafunzi waliomaliza mwaka 2018 walikuwa 57 kati ya hao 41 walipata daraja A, 15 walipata daraja la B na mmoja alipata C.

"Wanafunzi wanaomaliza mwaka huu wapo 51 wana nidhamu,  matumaini yetu mwaka huu hakuna mwanafunzi atakayepata alama C na tunatarajia kuwa kwenye 10 bora," amesema Shayo.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz