Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazazi waaswa kutoa elimu afya ya uzazi kwa watoto wa kike

Parents 3.jpeg Wazazi waaswa kutoa elimu afya ya uzazi kwa watoto wa kike

Sat, 20 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

WAZAZI mkoani Shinyanga, wameaswa kuwa wanatoa elimu ya afya ya uzazi mara kwa mara kwa watoto wao wa kike, ili kuwaepusha kupata mimba za utotoni na kukatisha ndoto zao.

Alisema ili Mkoa wa Shinyanga upate kupunguza matukio ya mimba za utotoni, ni vyema wazazi wavunje ukimya kwa kuzungumza na mabinti zao mara kwa mara, juu ya masuala ya afya ya uzazi na madhara ya kufanya ngono katika umri mdogo.

“Sisi katika utekelezaji wa mradi wetu Tunaweza, tunasaidia mabinti 100 ambao wana uzao mmoja katika kuwapatia elimu ya afya ya uzazi, pamoja na kuwajenga kiuchumi kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali, ili wapate vipato na kujitegemea katika maisha yao,”alisema Vigero.

“Mabinti hawa ukiangalia historia zao hawakupata kabisa elimu ya afya ya uzazi kutoka kwa wazazi wao, na hivyo wakajikuta wanaingia kwenye mahusiano na hatimaye kupata ujauzito bila matarajio na kuharibu ndoto zao, hivyo natoa wito kwa wazazi zungumzeni na watoto wenu msiwe bize na maisha,”aliongeza.

Naye mmoja wa wazazi Tausi Ferooz, alisema yeye binti yake hua anampatia elimu ya afya ya uzazi mara kwa mara, pamoja na kumfuatilia mienendo yake, na kutoa wito kwa wazazi wenzie wasiwe wavivu kuwalinda watoto wao, na watu ambao hutaka kuharibu maisha yao.

Mzazi mwingine ambaye (jina lake tumelihifadhi), alitoa wito kwa wasichana waachane pia na tamaa ya kutaka vitu vizuri, pamoja kujiingiza kwenye makundi mabaya, na kujitolea mfano yeye nyumbani kwao kulikuwa na kila kitu, lakini alijiingiza katika mambo yasiyo faa, akaambulia kupewa mimba ya utotoni.

Kwa upande wa wasichana hao, waliwatupia lawama wazazi kuwa baadhi yao wamekuwa chanzo cha watoto wao kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi, sababu ya kuwa bize na maisha, pamoja na wengine kushindwa kuwatimizia mahitaji yao na kuamua kujitafutia na hatimaye kunasa ujauzito

Chanzo: ippmedia.com