Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazazi wa wanafunzi watoro shuleni kusakwa

Mon, 25 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ukerewe. Msako wa kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wa wanafunzi watoro na waliopata mimba wilayani Ukerewe utaanza Machi, 2019.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe, Colonel Magembe ametoa agizo hilo jana Februari 22, 2019 alipokutana na walimu wakuuu wa shule za msingi na sekondari, maofisa elimu kwa ajili ya kupanga mikakati ya elimu.

Amesema ripoti ya kila miezi mitatu anayopewa inaonyesha wanafunzi wa sekondari wasiopungua 30 na 15 wa shule za msingi hukatiza masomo baada ya kupata ujauzito.

Amebainisha kuwa uchunguzi unaonyesha wanafunzi na walimu ni watoro na ndio sababu ya kurudisha nyuma shule nyingi kitaaluma.

Kutokana na uwepo wa jambo hilo ameagiza kupata orodha ya wazazi na walezi wa wanafunzi watoro na waliopata mimba ifikishwe ofisini kwake ili aweze kuchukua hatua.

“Ndugu zangu sitoweza kuvumilia hali hii kwa kuwa kila mwaka wilaya yetu inakuwa ya mwisho kimkoa katika matokeo ya mtihani wa kitaifa,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

Ametoa agizo hilo kufuatia ombi la mkuu wa Shule ya Msingi Msozi, Faustin Henry aliyeomba ufanyike msako wa wanafunzi watoro ikiwa ni mkakati wa kuinua taaluma.

 

Ofisa elimu Sekondari Wilaya ya Ukerewe, Venance Nyamwale amesema kila mwezi wanafunzi wanapimwa mimba na  wanaobainika kuwa na ujauzito huondolewa shuleni.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz