Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wanaswa na nyara za Sererikali Iringa

Kamatwa Pic Data Wawili wanaswa na nyara za Sererikali Iringa

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Polisi Mkoa wa Iringa inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo mawili mazima na vipande viwili vidogo kwenye mfuko wa ‘sulfate’ vyenye uzito wa kilo 65.

Watuhumiwa hao ambao ni mwanamke na mwanaume walikamatwa katika Kijiji cha Mapogoro kata ya Tungamalenga tarafa ya Idodi wilayani humo baada ya askari na raia wema kuweka mtego.

Akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja usiku wakati wakisubiri gari ya mnunuzi,ambapo watuhumiwa hao walikamatwa na wamefikishwa mahakamani kusomewa shtaka dhidi yao.

Bukumbi ameeleza kuwa katika tukio lingine maeneo ya posta kata ya Gangilonga, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya wanyamapori (RUAHA NATIONAL PARK) walimkamata mtuhumiwa mmoja mkazi wa Tungamalenga akiwa na akiwa na jino moja lenye urefu wa futi moja.

“Askari wakiwa kwenye msako baada ya kuweka mtego tulimkamata mwanaume mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa na jino moja lenye urefu wa futi moja akiwa analisafirisha toka Tungamalenga kuelekea Gangilonga kwa dhumuni la kufanya biashara na mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika”amesema Bukumbi

Kamanda Bukumbi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa mapema juu ya viashiria vya uhalifu wakati wote.

Advertisement “Katika kuelekea msimu wa sikukuu na mwaka mpya ulinzi utaimarishwa zaidi,wananchi muendelee kuwa watulivuna kuchukua tahadhali kwenye mali zenu na kuziba mianya ya uhalifu,wakati wa mkesha msiache nyumba bila uangalizi”

Kamanda Bukumbi ametoa onyo kwa madereva na wananchi wote kujiepusha na tabia iliyojitokeza ya ufungaji barabara na kufanya vurugu hususani kwa waendesha bodaboda wawpo kwenye sherehe mbalimbali kwani kitendo hiko ni kosa kwani husababisha usumbufu na kero kwa watumiaji wengine wa barabara.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz