Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wakamatwa kwa tuhuma za mauaji, dawa za kulevya

Nyundo Wawili wakamatwa kwa tuhuma za mauaji, dawa za kulevya

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewakamata watu wawili kwa tuhuma za usafirishaji wa dawa za kulevya na mauaji.

Wawili hao ni dereva bajaji, Peter Mwacha (18) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha ambaye amekamatwa akituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kilogramu 98.55, huku Ramadhani Yahaya (28) maarufu Msambaa akituhumiwa kwa mauaji.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justine Masejo leo Mei 31, 2024 imesema katika tukio la dawa za kulevya, Mwacha amekamatwa Mei 29, 2024, eneo la Elerai jijini hapa.

"Mtuhumiwa huyo amekamatwa akisafirisha dawa hizo kwa kutumia bajaji yenye namba za usajili MC 541 CXL aina ya TVS, tunakamilisha taratibu ili mtuhumiwa afikishwe katika vyombo vya sheria," amesema.

Kwa tukio la tuhuma za mauaji, Kamanda Masejo amesema jeshi hilo limemkamata Yahaya maarufu kwa jina la Msambaa ambaye anatuhumiwa kuhusika katika tukio la mauaji yaliyofanyika Mei mwaka huu eneo la Daraja mbili jijini Arusha.

"Nitoe wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za kweli za kihalifu kwenye vyombo vya dola au Serikali za mitaa. Msitoe taarifa kwenye mitandao zisizo za kweli kwani mnasababisha wahalifu kukimbia na kukwepa mkono wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuleta taharuki na hofu kwa wakazi na wageni wanaotembelea mkoa wetu," amesema.

Chanzo: Mwananchi