Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wajinyonga Njombe

Kujinyonga Pic Njombe Wawili wajinyonga Njombe

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: mwanachidigital

Watu wanne wamefariki dunia wakiwamo wawili wanaodaiwa kujinyonga na mmoja kunywa sumu mkoani Njombe.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani leo Alhamisi Novemba 3, 2022.

Kamanda Issah amesema katika vifo hivyo, watu wawili wamefariki dunia kwa kujinyonga, mmoja kunywa sumu huku kifo cha mwingine kikidaiwa kusababishwa na kipigo.

Amesema kuwa katika matukio hayo, ndugu wa mwanamke mmoja walidai kuwa alikunywa sumu kutokana na kukata tamaa baada ya kuumwa kwa muda mrefu huku mwanamke mwingine akijinyonga.

"Mmoja aliumwa kwa muda mrefu kiasi cha kukata tamaa na matokeo yake amechukua vichupa viwili vya sumu amekunywa na matokeo yake mama huyu kapoteza maisha" amesema Kamanda Issah.

Kamanda huyo amesema kuwa kifo kingine ni cha mzee wa mjini Makambako anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka sitini ambaye anadaiwa kujinyonga baada ya kutelekezwa na ndugu zake.

Amesema Jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji.

Chanzo: mwanachidigital