Watu wawili wanahofiwa kufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyotokea leo Agosti 5 katika barabara ya Buza, Mwisho wa lami ikihusisha lori la mafuta lililoacha njia na kupinduka.
Mashuhuda wameiambia Daily News Digital kuwa hiyo ni ajali ya pili kwa mwaka huu ikihusisha lori la mafuta kushindwa kukata kona na kupinduka. Hadi sasa (Saa 5:30 usiku) lori hilo bado halijaondolewa na kwamba halijashika moto.
Jeshi la Polisi na kikosi cha zimamoto na uokozi hakijazungumzia ajali hiyo. Hata hivyo Wakazi wa eneo hili wanasema ufinyu wa barabara, ongezeko la yadi na wafanyabiashara kando ya barabara kinaweza kuwa chanzo kikuu cha ajali katika eneo hilo ambalo linashuhudia ongezeko la magari na mengi yakiwa malori mabovu.