Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki wakichimba dhahabu

WACHIMBAJI Wawili wafariki wakichimba dhahabu

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamefariki dunia baada ya maji kujaa ndani ya mgodi wa dhahabu wa Kunanga ulioko eneo la Kinyambwiga wilayani Bunda mkoani Mara,

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vincent Naano watu hao wamekumbwa janga hilo Oktoba 17, 2023 baada ya mvua kubwa kunyesha na maji kujaa ndani ya shimo walilokuwepo wakati wa uchimbaji dhahabu.

Mkuu huyo wa wilaya pia amesimamisha uchimbaji katika mgodi huo kwa siku nne ili kupisha mamlaka za Serikali na uchimbaji kufanya ufuatiliaji na tathmini ya uimara wa mashimo hayo kisha shughuli za uchimbaji zitaendelea.

Baba mzazi wa mmoja wa marehemu hao, Mwita Mwita amesema amepokea taarifa za kijana wake kufariki kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live