Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki kwa kuangukiwa na ukuta Chato

Ukuta Chatooo.png Wawili wafariki kwa kuangukiwa na ukuta

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa kwa kuangukiwa na ukuta kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Chato Mkoani Geita.

Akitolea Ufafanuzi wa vifo hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Mganza James Kongwa amesema chanzo kinatokana na kuangukiwa na ukuta ambapo Mama na Mtoto wa miaka 6 wamevunjika mguu pamoja na Mtoto kuumia sehemu za kichwani.

Akiongea mbele ya RC wa Geita, Martine Shigela, Afisa Mtendaji huyo amesema “Nyumba nyingi zimeanguka na mpaka sasa hivi, Mkuu wa Mkoa tuna Watu wawili wamepoteza maisha waliangukiwa na ukuta lakini pia tunao Majeruhi tuna Watu watatu ambao walijeruhiwa kutokana kuangukiwa na ukuta”

RC Shigela ametembelea na kuona hali halisi katika eneo hilo na kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia kwa Wafiwa pamoja na Majeruhi wote huku akiwataka Wananchi wote waliojenga katika maeneo yanayopita maji kuhama huku akimuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chato kuhakikisha wote waliopatwa na majeraha wanapatiwa matibabu kwa uharaka zaidi bila malipo yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live